Kukeketwa (Female Genital Mutilation).
Kukeketwa
ni kitendo cha kukata sehemu ya uke hasa kisimi kwa wanawake. Katika
Afrika kuna nchi 28 ambazo hufanya hicho kitendo cha kikatili, na pia
nchi kama Yemen na Indonesia bado wanafanya.
Ingawa
wanawake waliokeketwa huweza kurudia hali ya kuweza kufika kileleni,
walio wengi huathiriwa sana na hiki kitendo na kuwasababishia
kushindwa kufika kieleleni.
Kuna
baadhi ya mitazamo na malezi ya dini, jadi au tamaduni huwapa
wanawake mtazamo mbaya, finyu na usio na maana kuhusiana na tendo la
ndoa.
Katika
dini, jadi, na tamaduni nyingi ukiacha jando na unyago, elimu ya
mwanamke kuhusu mwili na uzazi havifundishwa wala kutamkwa matokeo yake
wanawake wengi hawaijui miili yao, kiasi ambacho unakuta kijana wa
kiume anamuoa binti hajui chochote kuhusu mwili wa huyo mwanamke na
mwanamke mwenyewe hajui chochote kuhusu mwili wake mwenyewe, akiguswa
chuchu anakataa kwani ni kwa ajili ya mtoto, hapo utategemea afikishwa
kileleni kweli?
Kisaikolojia.
Hili huchangia kwa asilimia 95 kwa matatizo yote yanayosababisha mwanamke asifike kileleni.
Adui mkubwa anayetisha sana wa mwanamke kutofika kileleni ni akili (mind.)
Hofu
labda ya kuachwa, mashaka, kutojiamini, kukasirika, donge moyoni,
kisirani au mahusiano kutokuwa mazuri huweza kusababisha mwanamke
kutofika kileleni, Kushindwa ku- concentrate kwenye tendo lenyewe na
kupata hisia halisi (sensations).
Kuwa
na mawazo ya kitu kingine wakati wa tendo la ndoa Mawazo hasi
(Negative) kuhusu tendo la ndoa, pia Kuwa mchomvu kutamfanya mwanamke
asifike kileleni.