
Msanii na Mshiriki wa Big Brother GOLDIE HARVEY Amefariki Dunia Usiku wa Kuamkia Leo
Habari ya kushtusha iliyotokea usiku huu ni kwamba yule mshiriki wa Big
Brother Africa 2012 na mwanamuziki maarufu nchini Nigeria, Goldie Harvey
amefariki dunia.
Sio rahisi kuamini kwani Goldie ndo alishaianza safari ya mafanikio ya
kuwa msanii mkubwa hapa Afrika na kufanya kazi na baadhi ya wasanii
wakubwa ikiwemo Ambwene Yesaya kutoka Tanzania.
Taarifa inasema kuwa Goldie amefariki dunia usiku huu akiwa ndo amerudi
kutoka trip yake huko Marekani, chanzo kamili cha kifo cha mwanadada
huyu bado hakijawa wazi kwani tukio limetokea kwa ghafla sana usiku wa
kuamkia leo.