Kampuni ya Tanzania Music Power Entertainment ya jijini Dar es salaam ikishirikiana na Hotel Demag imeandaa tuzo kwa wapendanao kwa mwaka 2013.
Hizo ni tuzo za mara ya kwanza kufanyika nchini ambapo kwa mwaka huu zitawatuza wapendanao wawili walio mfano wa kuigwa katika jamii katika kudumu kwao katika mapenzi kwa kuvumiliana. Pia wapendanao hao wawe wameweza kwa pamoja kurudisha kwa jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo kutoa ajira au mchango mbalimbali kwa wahitaji.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Tanzania Music Power Entertainment, Phabian Duwe
akifafanua jambo wakati wa kutangaza tuzo za wapendanao zitakazofanyika
Februari 14 kwenye Hoteli ya Demag iliyopo Mwananyamala jijini Dar es
Salaam. Katikati ni Meneja wa TMPE, Evelyn Munisi na Ludovick Mugasha.
Kampuni hiyo itatoa tuzo hiyo ya The Best Couple 2013 kwa mtu yeyote katika jamii bila kujali itikadi yake ambapo anaweza kuwa mbunge,msanii wa muziki ama filamu, waziri ama mtu yeyote maarufu nchini.
“Mshindi wa tuzo hiyo atapatikana kupitia tafiti zetu katika vyombo vya habari mbalimbali,magazeti,runinga,radio,mitandao mbalimbali ya kijamii n.k ambaye kimsingi mshindi wa tuzo hiyo sharti anatakiwa awe hajaripotiwa vibaya au kuwa na skendo mbalimbali zinazomchafua,” imesema kampuni hiyo kwenye maelezo yake.
Mwanamuzi,
Rogers Lucas atakayetoa burudani katika utoaji wa tuzo hiyo. Kushoto ni
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Phabian Duwe na Meneja wa TMPE, Evelyn
Munisi.
0 comments