Pita pita ya paparazzi wetu zilinasa tukio hilo ndani ya ukumbi wa Travertine uliopo Magomeni jijini Dar es Salaam, ambako alimkuta kijana huyo akipepewa ili arudishe pumzi.
Ukurasa wa maelezo ya mashuhuda ulisomeka kwamba, kabla ya kipigo kijana
huyo alikuwa akitandika ‘maji makali’ na mwanamke mmoja
aliyemtambulisha kama ‘maiwaifu’ wake.
Inaelezwa, safisha koo ilipokolea, huduma ya upakuaji maji taka ilihitajika mwilini, ndipo jamaa huyo alipomuaga mkewe kwamba anakwenda maliwatoni kujihifadhi.
Dondoo zinaweka wazi kwamba, hatua chache baada ya kunyanyuka kwenye kiti, jamaa alikutana na msichana mdogo mweupe, ambaye alijikuta amemshika kiunoni, kwa tamaa au vinginevyo hilo halikuelezwa
.Inaelezwa, safisha koo ilipokolea, huduma ya upakuaji maji taka ilihitajika mwilini, ndipo jamaa huyo alipomuaga mkewe kwamba anakwenda maliwatoni kujihifadhi.
Dondoo zinaweka wazi kwamba, hatua chache baada ya kunyanyuka kwenye kiti, jamaa alikutana na msichana mdogo mweupe, ambaye alijikuta amemshika kiunoni, kwa tamaa au vinginevyo hilo halikuelezwa
Makelele ya ‘kaua, kaua’ yalipotawala ukumbini, baunsa alitimua mbio na kumuacha mke wa kijana aliyezimia akilia na kuomba msaada wa wasamaria, waliojitokeza na kumkimbiza majeruhi hospitali.
0 comments