Open top menu
Wednesday, February 13, 2013


IMANI ya jamii ya siri ya Freemasons imeonekana kuuteka Mji wa Moshi na vitongoji vyake kutokana na matangazo mengi kubandikwa kila kona yakihamasisha wafuasi kujiunga huku ofa ya utajiri ikipewa kipaumbele.
Risasi Mchanganyiko limeshuhudia matangazo mengi yanayohamasisha kujiunga na imani hiyo yakiwa yamebandikwa kila kona ya mji huu ikiwemo katika nguzo za umeme.
 
Hall la Masonic moshi
Katika tangazo hilo, wahusika wameeleza kwamba watakaojiunga mapema watapewa magari ya kifahari na nyumba za kisasa ikiwa ndiyo njia za awali za kubadilisha maisha yao.
Mwandishi wetu alijifanya anataka kujiunga na kupiga namba za simu zilizowekwa katika tangazo hilo ambazo ni 0783 127 967 ambapo ilipokelewa na mwanaume aliyekataa kutaja jina lake lakini alitoa masharti ya kujiunga.

“Tuma majina yako matatu; lako, baba na babu yako halafu tuma na shilingi 100,000 kwenye namba 0714 084 841 ambayo ni ada ya uanachama kisha utakwenda Kindoroko Hotel, chumba namba 87 hapo utakutana na bosi wangu na utaandikishwa rasmi na kupewa nguo zenye nembo yetu,” alisema mtu huyo.
Matangazo ya kujiunga na Freemason yakiwa yamebandikwa katika moja ya mti
Mwandishi wetu alifika katika Hoteli ya Kindoroko iliyopo mjini hapa juzi, Jumapili Februari 10, mwaka huu, akaonana na mtu wa mapokezi na kujitambulisha kama mwanachama mpya anayetaka kuonana na mhusika aliyepanga chumba namba 87.
Cha kushangaza, mhudumu alimwambia hawana mteja wa aina hiyo katika hoteli yao na kwamba hakuna chumba chenye namba aliyoelekezwa, jambo lililoonesha wazi kuwa wahusika ni matapeli wanaotaka kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.
Naye meneja wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Sara alipopigiwa simu, alitoa majibu kama ya mtu wa mapokezi.
Upekuzi wa gazeti hili umebaini kuwa, simu namba 0714 084841 iliyotakiwa kutumiwa fedha na mtu aliyejiita wa Freemasons imesajiliwa kwa jina la Flora Tuvana.
SOURCE:GPL
Tagged
Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments