Habari ya kushtusha iliyotokea usiku huu ni kwamba yule mshiriki wa Big
Brother Africa 2012 na mwanamuziki maarufu nchini Nigeria, Goldie Harvey
amefariki dunia.
Sio rahisi kuamini kwani Goldie ndo alishaianza safari ya mafanikio ya
kuwa msanii mkubwa hapa Afrika na kufanya kazi na baadhi ya wasanii
wakubwa ikiwemo Ambwene Yesaya kutoka Tanzania.
Taarifa inasema kuwa Goldie amefariki dunia usiku huu akiwa ndo amerudi
kutoka trip yake huko Marekani, chanzo kamili cha kifo cha mwanadada
huyu bado hakijawa wazi kwani tukio limetokea kwa ghafla sana usiku wa
kuamkia leo.
Kwenye Facebook page na Twitter ilitumwa taarifa hii na admin wake wa
account hizo, “It is with heavy heart that I have to inform you all that
Goldie passed this night shortly after arriving Lagos from LA. May her
soul rest in the eternal peace of the Lord – Admin!!”.
Goldie ambaye jina lake asilia ni Susan Oluwabimpe Harvey alipewa jina
la "Goldie" kwasababu ya rangi asili ya nywele zake ambayo ni ya Dhahabu
(Golden).
SOURCE: http://www.facebook.com/GoldieHarveyBigBrotherStarGame
0 comments