DUNIANI kuna mambo; wadau wa tasnia ya filamu nchini wameibua minong’ono inayodai kuwa kampuni maarufu ya kusambaza kazi za wasanii Bongo ya Steps Entertainment ya jijini Dar es Salaam, eti inatumia hirizi kuwapumbaza wasanii.
Ushahidi uliowekwa hivi karibuni mezani kwenye dawati la Amani na mmoja wa wasanii nguli nchini ni uwepo wa kitu cheusi kinachohisiwa kuwa ni ‘king’amuzi’ cha jadi kinachoning’inia juu ya usawa wa mlango wa kuingilia ndani ya kampuni hiyo.
“Wanatumia dawa, msanii unaweza kuondoka nyumbani na hasira lakini ukifika hapo unapoa,” alisema msanii huyo.
Hata hivyo, timu yetu ilishindwa kutambua kinagaubaga kama kitu hicho ni hirizi au ni sanaa iliyowekwa mlangoni kwa kazi maalumu ambayo msemaji wa kampuni hiyo hakuweza kupatikana, huku wafanyakazi wengine wakisita kusema chochote
0 comments