LICHA ya afya ya msanii wa vichekesho nchini, Tumaini Mwakibibi
‘Matumaini’ kuonekana kuendelea vyema na kuruhusiwa kutoka katika
hospitali ya Amana jijini Dar, Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji nchini,
Michael Sangu ‘Mike’ amewataka wadau kumsaidika ili afanyiwe uchunguzi
zaidi.
Mike aliyasema hayo hivi karibuni alipoongea na Tollywood Newz na
kubainisha kuwa Matumaini anatakiwa afanywe uchunguzi wa figo na ini ili
aweze kupona kisawasasawa.
“Ingekuwa vyema kama tungejitolea kumsaidia apate vipimo kwenye
hospitali kubwa, kwani amerudishwa nyumbani lakini siyo mtu mwenye hali
ya kuridhisha, anayetaka kumsaidia atumie namba 0718 951 355,” alisema
Mike.
0 comments