KUTOKANA na vifo vya mfululizo vya wasanii, msanii wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ ameamua kumrudia Mungu kwa kutoa zawadi za vitabu vya dini msikitini.
Tukio hilo lililopigwa chabo na papaarazi wetu lilitokea Novemba 27, mwaka huu katika Madrasa za Mukaddamati, Al- Hillal A na B, Nurain na Msikiti wa Muzdalifat, Mikocheni A jijini Dar ambapo Baby Madaha aliambatana na meneja wake, Mercy Kayuni kwenda kutoa zawadi hizo.
“Ni vyema tukiishi kwa kumkumbuka Mungu kila wakati, maana hatujui siku wala saa za kuishi hapa duniani. Leo tumejaliwa kutoa misahafu mitano na juzuu 250,” alisema Baby Madaha.
Mbali na kutoa zawadi za vitabu hivyo vya dini, Baby Madaha aliombewa dua na wanafunzi wa madrasa hizo kila alipomaliza kutoa zawadi hizo.
Aidha, imamu wa wa msikiti wa Muzdalifat, Ustadhi Hajj Issa Hemed aliwataka wasanii wengine kuiga mfano huo kuliko kupoteza fedha nyingi katika mambo yasiyo na msingi.
0 comments