Open top menu
Friday, December 14, 2012

MSANII wa filamu ambaye pia anafanya muziki, Zuena Mohammed ‘Shilole’  na demu mwenzake aliyefahamika kwa jina la Hawa Juma ‘Mama Ayana’ hivi karibuni waliwaacha watu midomo wazi baada ya kugandana kimahaba mbele za watu.
Tukio hilo lilitokea Msasani jijini Dar kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi ambako kulikuwa na pati ya kusherehekea kuzaliwa kwa Hawa.
Wakiwa eneo hilo, wawili hao walionekana kuwa karibu sana na lilipofika zoezi la kulishana keki na kufika zamu ya Shilole aliyekuwa MC, Hawa aliweka pembeni ‘stiki’ aliyokuwa akiitumia kulishia watu wengine kisha kutumia mdomo wake kumlisha msanii huyo.


                          Shilole na Hawa wakisogeleana kimahaba.

 
Zuena Mohammed ‘Shilole’ na Hawa Juma ‘Mama Ayana’ wakiwa wamegandana kimahaba.
Kitendo cha wawili hao kugandishiana midomo yao huku wakionekana wenye hisia, kilichukua muda wa takriban sekunde 60, mazingira yaliyowafanya baadhi ya waalikwa kuanza kunong’ona kuwa, kilichofanyika ni usagaji.
“Dah! Ndiyo nini sasa vile anafanya mama Ayana, mi’ sijapendezewa, watu si watahusisha na mambo ya usagaji,” alisikika akisema mama mmoja wa makamo.
 
 Zuena Mohammed ‘Shilole’.
Hata hivyo, wenyewe walipozungumza  kwa nyakati tofauti walisema kuwa, walichokifanya si kitu cha ajabu. Aidha, taarifa zilizopatikana baadaye zinadai kuwa mwanaume ambaye amejiweka kwa mama Ayana (jina kapuni) alipopewa taarifa za tukio hilo alifura kuonesha kutofurahishwa nalo.

Tagged
Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments