Details: Baada ya kusubiriwa kwa hamu kubwa ,documentary ya kwanza ya ya
wimbo wa hip hop Tanzania BUM KUBAM DVD inayomhusisha Nikk wa pili, G
nako, Bontha na watu wengine maarufu kama Adam mchomvu, sam misago,
Millard ayo, Adamu Juma itakua mtaani kuanzia tarehe 21/12/12.
BUM KUBAM DVD itasambazwa kwa mfumo mpya kabisa wa code namba
uliopewa jina la MFUMO RAFIKI na utaanza kutumika rasmi tarehe 21/12/12
FAIDA ZA MFUMO RAFIKI
1. Msanii anaunganishwa moja kwa moja na mfumo na kuona idadi ya nakala zote alizouza, muda na mahali zilipouzwa.
2. Unazuia wauzaji feki kuuza kazi ya msanii.
3. Msanii atamfahamu kila mtu aliyenunua bidhaa yake na kuwasiliana nae moja kwa moja.
4. Wezi wote wa kazi ya msanii watajulikana hadharani.
5. Kazi ya msanii itapatikana kwa urahisi na kwa wakati.
6. Unapunguza vichocheo vya piracy kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa maelezo zaidi ni siku ya uzinduzi wa mfumo huu mpya tarehe 21/12/12.
Ahsante kwa ushirikiano wako.
Friday, December 14, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments