Open top menu
Monday, December 17, 2012




MKATA mayenu wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Grace Utete ‘Kiza Kinene’ juzikati alianza maandalizi ya kufunga mwaka vibaya baada ya kupewa talaka mbili na mumewe aliyetambuliwa kwa jina moja la Abeid.

Tukio hilo lililoshuhudiwa na mapaparazi wetu, lilijiri mchana kweupe katika Baa ya Ben Kinyaiya iliyopo Kinondoni, Dar huku mkurugenzi wa bendi anayowajibika mnenguaji huyo, Asha Baraka na meneja wake, Khamis Kayumbu ‘Amigolas’ wakishuhudia. Baada ya mnenguaji huyo kupokea talaka, Ijumaa Wikienda

lilimvaa na kumuuliza kulikoni kupewa talaka baa, tena mbele ya viongozi wake ambapo bila hata kupepesa macho alijibu kuwa haoni tatizo na kwamba anaifurahia hali hiyo. Hadi Ijumaa Wikienda linaondoka eneo la tukio, Asha Baraka alikuwa amekaa kikao na aliyekuwa mume wa mnenguaji huyo lakini haikujulikana kikao hicho kilihusu nini.
Tagged
Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments