MWANADADA anayetisa katika tasnia ya filamu Nchini Irene Uwoya anasema kuwa mwaka 2012 unamalizika huku akiwa na ndoto zake kubwa katika tasnia ya filamu ambazo kwa asilimia fulani anaamini hajazikamilisha hivyo anatarajia kufanya mambo makubwa kwa mwaka 2013 kuanzia January rasmi ataanza kutekeleza mipango yake ya uandaaji wa filamu.
“Kwa sasa kuna changamoto nyingi sana katika tasnia ya filamu ambazo kama msanii unatakiwa kuzikabili katika kulinda maslahi na kupunguza muda mwingi wakuwa shooting na kukosa muda wa kupumzika na kufikiria filamu mpya ambayo itakuwa bora,”anasema Irene Uwoya.
Irene anasema moja ya njia ya kuongeza maslahi kwa msanii wa filamu ni pamoja na kumiliki kampuni itakayojishughulisha na kazi ya kurekodi filamu na kufanya kazi za kampuni yake kwakiwango kikubwa, kwa sasa watayarishaji wengi wanajitahidi kumiliki kampuni za utengenezaji wa filamu katika kujiongezea maslahi zaidi.
0 comments