lulu akisindikizwa na askari Magereza.
WAKATI Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Zainabu Mruke
akimwachia Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael Kimemeta (Lulu) kwa
dhamana yenye masharti matano ,Msajili wa Mahakama Kuu Amir Msumi amekwamisha dhamana ya msanii huyo na kumlazimu kurudi rumande mpaka kesho.Kwa muujibu wa taarifa zilizonaswa na Habarimpya.com hivi punde zinadai kwamba Lulu amerudishwa mahabusu kwa sababu msajili wa mahakama hiyo yuko Bagamoyo kikazi na anatarajia kurudi ofisini kesho.
"Lulu awezi kurudi nyumbani ingawa ametimiza masharti ya dhamana, kwa sababu msajili wa mahakama ambaye ndiye mwenye mamlaka kisheria ya kuidhinisha dhamana yake ayupo ofisini".
"Hakuna mwenye mamlaka ya kumruhusu tena, ila kesho atakuwepo ofisini na Lulu atatakiwa kurudi Mahakamani tena kwa ajili ya kuja kusaini dokomenti zake za dhamana mbele ya Msajili wa Mahakama hiyo" kilisema chanzo chetu ndani ya Mahakama hiyo.
Akisoma uamuzi wa maombi ya dhama ya msanii huyo Jaji Mruke alisema, "Mahakama imekubali maombi yako ya dhamana na uko huru kwa masharti yafuatayo, (moja) unatakiwa kuwasilisha gharama zote za safari ndani ya jiji la Dar es Salaam".
"(Pili) usisafiri nje ya Dar es Salaam bila idhini ya Msajili wa Mahakama Kuu, (tatu) unatakiwa kuripoti (kujiwakilisha) kwa Msajili wa Mahakama kila tarehe mosi ya kila mwenzi".
Akisoma uamuzi wa maombi hayo Jaji Mruke alifafanua kuwa, "Sharti la (nne) unatakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaofanya kazi serikalini na wawe na tsh 20milioni kila mmoja".
"(Tano) ni kwamba unatakiwa kutimiza masharti ya dhamana na kusaini mbele ya msajili wa Mahakama na utaendelea kubaki rumande mpaka utakapotimisha masharti yote".
Source:Mwanahabari Mpya
0 comments