Open top menu
Tuesday, January 22, 2013


Ilikuwa ni Sinza mama huyu alitupwa nje ya nyumba baada ya kuvamiwa na mabaunsa chini ya usimamizi wa polisi.Ambapo mama huyu alisema mtu aliyenyuma ya tukio hilo ni aliyekuwa mume wake.

Akisimulia Mkasa anasema yeye na huyo aliyekuwa mume wake wamekuwa na mvutano juu ya hiyo nyumba.Alioana na mumewe mwaka 1998 na kuhamia katika hiyo nyumba mwaka 2000.Mwaka 2007 ndio migogoro ilipoanza baada ya mwanaume kuanza kutokurudi nyumbani na hatimae kutokurudi kabisa.Katika ndoa hiyo wana watoto watatu.Kwa muda wote mume amekuwa akitaka kumtupa nje na watoto wa kigezo kuwa hiyo nyumba sio yake mwenyewe anaitaka.Siku ya tukio jana yake mume alikuja akawachukua watoto akisema anaenda kuwanunulia vifaa vya shule hakuwarudisha.Asubuhi mama anashangaa watu wanaruka ukuta na kuvunja milango kumbe wamekuja mabaunsa na polisi kuwatupa nje.

Tukafatilia kwa kumpigia kamanda wa polisi kanda ya Kinondoni na mkuu wa kituo cha polisi osterbay ambako polisi walitoka huko kusimamia zoezi la kuhamishwa mama huyu.Tukaambiwa wao walipata barua kutoka mahakamani kuwa wanahitajika kusimamia ulinzi wakati mpangaji wa nyumba hiyo akitolewa nje.Mwanasheria wa huyo mama anasema wana kesi mahakamani kati yake na huyo mume ambayo haijaisha na inatarajiwa kusikilizwa kwa mara ingine tarehe 2 mwezi ujao.Na mbaya zaidi yeye hajapewa taarifa kuwa ahame ila amevamiwa.
Vitu mbali mbali vikiwa nje baada ya kutolewa nje na ndani kuwekwa mabaunsa kulinda asiingie mtu.
Kama kuna kitu kiliniuma ni huyu bibi pichani.Huyu ni mama wa huyo dada na bibi wa watoto hao ambao walikuwa likizo muda wote shule zilipofunga.Bibi ndio alikuwa amewaleta wajukuu zake na kuishia kushuhudia mwanae akitupwa nje na mabaunsa akiwemo na yeye ni udhalilishaji wa hali ya 
Majirani wote walikuwa na huyo mama hasa wanawake wakiongea kwa jazba juu ya mkasa huo.Wakieleza jinsi gani hakupaswa kumfanya hivyo mtu aliyezaa nae watoto tena watatu na wote walikuwa wakiishi na mama yao.
Jioni majirani wakamsaidia kuhifadhi vitu kwenye nyumba zao
Mwenye kubeba kabati,vifurushi vya nguo,vyombo ilimradi wamsitiri mwanamke mwenzao.
Usiku majirani walifanya fujo sana kiasi cha mapolisi kuingilia kati...ishu ilikuwa huyo anaedai ndio mwenye nyumba ajitokeze.Alikuja mpaka diwani wa eneo hilo polisi pia wakaja kuwatoa hao mabaunsa na mama wa watu kurudishwa ndani ya nyumba.
Jana aliamkia mahakamani na mahakama kuamua akae kwenye hiyo nyumba bila kubugudhiwa mpaka kesi yao itakapo kwisha
Tagged
Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments