Martha Karua |
Martha Wangari Karua
ALIZALIWA TAREHE 22 SEPTEMBA MWAKA 1957 MKOA
WA KATI. NA YEYE NDIYE MGOMBEA WA PEKEE MWANAMKE KATIKA UCHAGUZI HUU.
ALIAJIRIWA KAMA HAKIMU AKIWA NA UMRI WA MIAKA 24 KABLA YA HATA KUWA
MBUNGE MIAKA KUMI BAADAYE.
MGOMBEA WA MUUNGANO WA NATIONAL RAINBOW COALITION
(NARC-KENYA), KARUA ALIMTEUA MWANAUCHUMI AUGUSTINE CHEMONGES LOTODO
KAMA MGOMBEA MWENZA WAKE. LOTODO PIA AMEWAHI KUWA MBUNGE KATIKA BUNGE
LA AFRIKA MASHARIKI
KARUA MWENYE UMRI WA MIAKA 55, ALIKUWA MWANACHAMA
WA UPINZANI AMBAO WALIPIGANIA SIASA ZA VYAMA VINGI NCHINI KENYA MAPEMA
MIAKA YA TISINI CHINI YA UTAWALA WA RAIS MSTAAFU DANIEL MOI ALIYEKUA
ANAONGOZA KIMABAVU CHINI YA CHAMA KIMOJA.
MKEREKETWA WA DEMOKRASIA NA MASWALA YA WANWAKE
NCHINI KENYA, KARUA ALIHUSIKA NA KUPIGANIA HAKI ZA WANAWAKE KWA KUTAKA
UUNGWAJI MKONO KATIKA MASWALA YANAYOWAHUSISHA WANAWAKE WENYEWE.
KARUA ALIKUWA MFUASI MKUBWA WA RAIS MWAI KIBAKI
NA SERA ZAKE HADI TAREHE SITA APRILI MWAKA 2009 WAKATI ALIPOJIUZULU
KAMA WAZIRI WA SHARIA, AKIELEZEA KUWA KAZI YAKE ILIKUWA INAINGILIWA
SANA NA BAADHI YA MAAFISA WAKUU SERIKALINI.
ALIONGOZA UPANDE WA SERIKALI WAKATI WA MAPATANO
KATI YA RAILA ODINGA NA KIBAKI ILI KUMALIZA GHASIA ZA BAADA YA UCHAGUZI.
PIA ALIWAHI KUHUDUMU KAMA WAZIRI WA MAJI ALIYEPIGIA
DEBE SANA SHERIA YA MAJI YA MWAKA2002 AMBAYO ILICHOCHEA MAGEUZI KATIKA
SEKTA HIYO.
KARUA ANAAHIDI KULETA MAGEUZI KATIKA SEKTA YA
AFYA, ELIMU, UONGOZI BORA KUBUNI NAFAS ZA KAZI, KUHUSISHA VIJANA KATIKA
MASWALA YA UONGOZI NA KUHAKIKISHA SERIKALI YAKE INAFANYA KAZI KUBORESHA
MAISHA YA WANANCHI.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,
Martha Karua. Kwa nini anagombea?
MARTHA KARUA, MWANAMKE PEKEE ANAYEGOMBEA URAIS,
ANAJIAMINI KUWA ANAWEZA KUSHINDA UCHAGUZI HUU, BAADA YA KUJITOKEZA KAMA
MTU MWENYE ARI KUTAKA KUSHINDA.
HILO LILIJITOKEZA KATIKA MJADALA WA WAGOMBEA
WA URAIS ULIOFANYIKA JUMATATU JIONI.
ALIJITOSA UWANJANI NA WAGOMBEA WENGINE WANANE
WAKIWEMO, RAILA ODINGA NA UHURU KENYATTA.
NA MWISHONI ALIWEZA KUWAHAKIKISHIA WAKENYA KUWA
WANAWEZA KUMUAMINI.KARUA ALIKUWA WAZIRI ALIYESIFIKA KWA UJASIRI WAKE
KISIASA INGAWA BAADAYE ALIJIUZULU KUTOKA KWA WADHIFA HUO. JOHN NENE
ALIZUNGUMZA NAYE KUJUA NINI KINAMSHAWISHI KUWA ANAWEZA KUSHINDA UCHAGUZI.
Uhuru Muigai Kenyatta
NAIBU WAZIRI MKUU WA KENYA TANGU MWAKA 2008,
UHURU KENYATTA, ALIZALIWA TAREHE 26 OKTOBA MWAKA 1961 KWA MAMA NGINA
NA MZEE JOMO KENYATTA, AMBAYE ALIKUWA RAIS WA KWANZA WA KENYA, KATI
YA MWAKA 1964-1978, NA AKAITWA "UHURU", NENO LA KISWAHILI
LINALOMAANISHA UKOMBOZI KUTOKA KWA WAKOLONI.
MRITHI WA MASHAMBA MAKUBWA KENYA,
ANATAJWA KUWA NAMBARI 23 KATIKA ORODHA YA WATU MATAJIRI ZAIDI AFRIKA
AKIWA NA THAMANI YA DOLA MILIONI MIATANO.
UHURU, ANAYEJULIKANA NA WAFUASI
WAKE KAMA "NJAMBA" NENO LA KIKIKUYU, LINALOMAANISHA, SHUJAA,
NI MGOMBEA WA URAIS WA MUUNGANO WA JUBILEE, AMBAO NI MUUNGANO WA VYAMA
VYA TNA CHAKE KENYATTA, (URP) NA (NARC). MGOMBEA MWENZA WAKE NI WILLIAM
RUTO WAKISAIDIANA NA CHARITY NGILU,
MWALIMU WAKE WA SIASA AMBAYE
NI RAIS MSTAAFU, DANIEL MOI ALIMUINGIZA KATIKA SIASA KWA MARA YA KWANZA
NA KUMPENDEKEZA KUWA MGOMBEA WA URAIS LICHA YA KUTOKUWA NA UZOEFU WA
KISIASA WAKATI WA UCHAGUZI WA MWAKA 2002.
HATA HIVYO, UHURU ALISHINDWA
PAKUBWA NA MPINZANI WAKE, RAIS MWAI KIBAKI NA HIVYO KUMFANYA KUWA KIONGOZI
RASMI WA UPINZANI BUNGENI.
UHURU ALIUNGANA NA RAILA KUPINGA
RASIMU YA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA NA KIBAKI MWAKA 2005, LAKINI BAADAYE
WAKATENGANA HUKU UHURU AKIMUUNGA MKONO KIBAKI KATIKA KUGOMBEA MUHULA
WA PILI.
KIBAKI, ALITANGAZWA MSHINDI KATIKA
UCHAGUZI ULIOKUMBWA NA UTATA MKUBWA NA PUNDE BAADAYE AKAMTEUA UHURU
KAMA WAZIRI WA SERIKALI ZA MITAA.
BAADA YA KIBAKI NA ODINGA KUTIA
SAINI MAKUBALIANO KUSITISHA MAPIGANO, UHURU ALITEULIWA KAMA MMOJA WA
MANAIBU WAWILI WA WAZIRI MKUU NA KISHA BAADAYE AKATEULIWA KUWA WAZIRI
WA FEDHA. LAKINI ALIJIUZULU BAADAYE BAADA YA KUPATIKANA NA MAKOSA YA
KUJIBU KATIKA KESI YAKE ICC YA UHALIFU WA KIVITA KUHUSU GHASIA ZA BAADA
YA UCHAGUZI MWAKA 2007.
KENYATTA ATAFIKA MAHAKAMANI BAADA
TU YA UCHAGUZI WA MWEZI MACHI, KWA KOSA LA UHALIFU WA KIVITA ICC. MGOMBEA
MWENZA WAKE, WILLIAM RUTO, PIA ANAKABILIWA NA MAKOSA HAYOHAYO.
ICC, INAMTUHUMU KWA KUPANGA MASHAMBULIZI
YALIYOFANYWA NA KUNDI HARAMU YA MUNGIKI, KUFANYA MASHAMBULIZI YA KULIPIZA
KISASI DHIDI YA KABILA LA WJALUO BAADA YA WALE WA KABILA LAKE WAKIKUYU
KUSHAMBULIWA KATIKA MKOA WA RIFT VALLEY.
RUTO NA UHURU WALIJITETEA VIKALI
DHIDI YA TUHUMA ZA ICC, NA KUSEMA KUWA WAZIRI MKUU RAIL ODINGA ANAPASWA
KUWAJIBIKIA GHASIA ZILIZOTOKEA BAADA YA UCHAGUZI MWAKA 2007/2008
KAMA WAZIRI WA FEDHA, KENYATTA
ALIKUWA KATIKA MSITARI WA MBELE KULETA MAGEUZI KATIKA WIZARA YA FEDHA
NA AMBAVYO SERIKALI HUFANYA BIASHARA ZAKE. HASA KATIKA KUPANGA MAKADIRIO
YA MATUMIZI YA PESA ZA SERIKALI KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII.
ALIKUWA WAZIRI WA KWANZA WA KENYA
KUZINDUA RUWAZA ILIYOUNDWA KWA KUHUSISHA WANANCHI NA KUTILIA MKAZO KATIKA
KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA UUNDAJI WA SERA ZA CHAMA CHAKE.
KENYATTA ANAAHIDI KULETA MAGEUZI
YA KIJAMII,KISIASA NA KIUCHUMI NA ANAWAALIKA WAKENYA WOTE KUHUSIKA NA
UUNDAJI WA SERA ZA CHAMA CHAKE.
PIA ANAAHIDI KUTOA HEKARI MILIONI
MOJA YA MASHAMBA KWA AJILI YA UKULIMA WA UNYUNYIZIAJI MAJI MIMEA NA
KUPANUA KILIMO KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,
Raila Amolo Odinga
RAILA ODINGA ALIZALIWA JANUARI TAREHE 7 MWAKA
1945 MAGHARIBI MWA KENYA MKOA WA NYAZA. RAILA, ANAYEJULIKANA KWA WAFUASI
WAKE KAMA "AGWAMBO" KUMAANISHA MWENYEKITI KWA LUGHA YAKE ASILI
YA DHOLUO, NI WAZIRI MKUU WA KWANZA WA KENYA , WADHIFA ULIOUNDWA KUFUATIA
MKATABA WA KITAIFA ULIOAFIKIWA BAADA YA GHASIA ZA BAADA YA UCHAGUZI
MWAKA 2007-2008 KAMA ISHARA YA KUGAWANA MAMLAKA.
ALITIA SAINI MKATABA WA KUGAWANA
MAMLAKA NA RAIS MWAI KIBAKI ILI KUMALIZA GHASIA ZA MIEZI MIWILI ZILIZOKUMBA
NCHI BAADA YA UCHAGUZI ULIOKUMBWA NA UTATA.
RAILA MWENYE UMRI WA MIAKA 68
WA CHAMA CHA ODM INGAWA KWA SASA ANAGOMBEA URAIS KWA MUUNGANO WA CORD,
AMEAMUA KUSHIRIKIANA NA MAKAMU WA RAIS KALONZO MUSYOKA, AMBAYE PIA ALIKUWA
HASIMU WAKE MIEZI MIWILI TU KABLA YA UCHAGUZI WA MWAKA 2007.
ALIONDOKA KUTOKA CHAMA CHA ODM
NA KUUNDA CHAMA CHAKE ODM-KENYA NA HATA KUITIKIA UTEUZI WAKE KAMA MAKAMU
WA RAIS WA SERIKALI YA RAIS MWAI KIBAKI.
KAMA HAYATI BABAKE, JARAMOGI
OGINGA ODINGA, RAILA AMBAYE NI WAZIRI MKUU WA KWANZA WA KENYA, KWA MIAKA
MINANE ALIISHI KUKAMATWA NA KUACHILIWA MARA KWA MARA TANGU MWAKA 1982
HADI 1991 KWA HARAKATI ZAKE ZA KUPIGANIA MAGEUZI WAKATI WA MUHULA WA
PILI WA UTAWALA WA RAIS DANIEL ARAP MOI.
KUFUATIA KUUNDWA KWA KATIBA MPYA,
MWEZI AGOSTI, MWAKA 2010, AMEKUWA AKISEMA KWENYE KAMPEINI ZAKE KUWA
NIA YAKE NI KULETA MAGEUZI YA KISIASA.
RAILA NI MWANASIASA ANAYESIFIKA
SANA KWA USHAWISHI WAKE KISIASA NA AMBAYE AMEKUWA KATIKA MSITARI WA
MBELE KUUNDA VYAMA VYA MIUNGANO NA WANASIASA AMBAO NI MAHASIMU WAKE.
BAADA YA UCHAGUZI WA MWAKA 1997
AMBAPO RAILA ALISHIKILIA NAFASI YA TATU, KUFUATIA KUUNDWA KWA MUUNGANO
WA CHAMA CHAKE (NDP) NA CHAMA CHA RAIS WA ZAMANI DANIEL MOI (KANU),
ALITEULIWA KAMA WAZIRI WA KAWI KATIKA SERIKALI YA MUHULA WA MWISHO WA
MOI.
MWAKA 2002, BAADA YA MOI KUMUUNGA
MKONO UHURU KENYATTA, KAMA MRITHI WAKE, RAILA NA MAAFISA WENGINE WA
KANU IKIWEMO KALONZO MUSYOKA NA WAFUASI WENGINE, WALIPINGA UNGWAJI MKONO
WA KENYATTA KUGOMBEA URAIS. WALIUNGANA NA KIONGOZI WA UPINZANI MWAI
KIBAKINA NA KUUNDA MUUNGANO WA NATIONAL RAINBOW COALITION (NARC) AMBAO
BAADAYE ULISHINDA UCHAGUZI WA MWAKA 2002.
MWAKA 2005 ALIUNGANA NA UHURU
KENYATTA ALIYEKUWA KAMA KIONGOZI RASMI WA UPINZANI, ILI KUSHINDA KURA
YA MAONI KUHUSU RASIMU YA KATIBA CHINI YA SERIKALI YA RAIS KIBAKI .
WAKATI KIBAKI ALIPOMFUTA KAZI
NA WASHIRIKA WAKE, ALIUNDA CHAMA CHA ODM AMBACHO KILIPIGA KURA YA LA
DHIDI YA RASIMU YA KATIBA MPYA. ALIONGOZA KAMPEINI MWAKA 2007 NA KWA
SHINGO UPANDE KUKUBALI USHINDI WA RAIS KIBAKI
KATIKA UCHAGUZI ULIOKUMBWA NA
UTATA , GHASIA NA MAUAJI. LAKINI HATIMAYE ALILAZIMIKA KUJIUNGA NA KIBAKI
KATIKA SERIKALI YA MUUNGANO.
DISEMBA MWAKA 2012, RAILA ALILAZIMIKA
KUPIGA MOYO KONDE NA KURUDIANA NA KALONZO MUSYOKA CHINI YA MUUNGANO
WA CORD, KWANI DAIMA HUSEMA KATIKA SIASA, HAKUNA MAADUI WA KUDUMU.
RAILA ANAAMINI KUWA WAKENYA WANASTAHILI
KUHUDUMIWA VYEMA ZAIDI KULIKO AHADI WANAZOPEWA NA KWAMBA CHINI YA UTAWALA
WAKE, RAILA ANAAHIDI KULETA MAGEUZI NA KUHAKIKISHA UONGOZI BORA. ANAAHIDI
KUWA SERIKALI YAKE ITAEKEZA KATIKA VIWANDA VYA KISASA , MABOHARI PAMOJA
NA VITUO VYA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO KATIKA MAENEO YA KUVULIA, USHIRIKIANO
NA SEKTA YA KIBINAFSI ILI KUIMARISHA KILIMO.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,
Wycliffe Musalia Mudavadi:
ALIZALIWA TAREHE 21 SEPTEMBA MWAKA 1960 MAGHARIBI
MWA KENYA KUTOKA JAMII YA WALUHYA.
MWANASIASA HUYU MWENYE UMRI WA MIAKA 52, NA AMBAYE
SIASA ZAKE HAZICHANGAMSHI SANA IKILINGANISHWA NA WANASIASA WENGINE,
NA WENGI WAKISEMA NI KWA SABABU YA ALIVYOLELEWA NA WAZAZI WAKE KATIKA
MISINGI YA KIDINI SANA.
MUDAVADI ALIMTEUA ALIYEKUWA MBUNGE JEREMIAH KIONI
KUTOKA MKOA WA KATI KAMA MGOMBEA MWENZA WAKE KATIKA CHAMA CHAO CHA MUUNGANO
WA AMANI.
VYAMA VILIVYO KATIKA MUUNGANO HUO, NI KUMI NA
TATU KIKIWEMO CHAMA CHA KANU CHAKE RAIS MSTAAFU DANIEL MOI. WADADISI
WANASEMA KUWA KUIBUKA KWA CHAMA HIKI HUENDA KUKASABABISHA DURU YA PILI,
YA UCHAGUZI NA WACHANGANUZI WANASEMA MUUNGANO WA AMANI UTAKUWA CHANGAMOTO
KWA AZMA YA KENYATTA NA RAILA.
MUDAVADI ALIKUWA MMJA WA MAWAZIRI WAKUU WAWILI
WALIOTEULIWA KATIKA SERIKALI YA MUUNGANO KATI YA RAILA NA KIBAKI KUFUATIA
MKATABA WA AMANI ULIOFIKIWA BAADA YA GHASIA ZA UCHAGUZI.ALIKUWA MGOMBEA
MWENZA WA RAILA ODINGA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 2007 KABLA YA KUJIUZULKU
ILI KUGOMBEA URAIS MWAKA HUU.
MUDAVADI PIA ALIKUWA MGOMBEA MWENZA WA UHURU KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 2002, LAKINI HATA AKASHINDWA KATIKA ENEO LAKE.
HATA HIVYO ALIFUFUA TENA AZMA YAKE YA KUGOMBEA MWAKA 2005 WAKATI WA
KURA YA MAONI KUHUSU KATIBA MPYA ALIPOKUWA NA UPANDE WA (LA) AMBAO ULISHINDA
DHIDI YA UPANDE WA KIBAKI ULIOKUWA UNAUNGA MKONO RASIMU YA KATIBA MPYA.
MUDAVADI ANASEMA KUWA SERIKALI YAKE, ITAKUWA KATIKA MSTARI WA MBELE
KULETA MAGEUZI MAKUBWA KATIKA MFUMO WA SIASA PAMOJA NA KUINUA UCHUMI
KWA MANUFAA YA WAKENYA WOTE.
ALISEMA WATABDILI MFUMO WA KUTOZA KODI, PAMOJA NA USAMBAZAJI WA RASILIMALI,
KUHAKIKISHA WAKENYA WOTE WATAWEZA KUPATA MSAADA WANAOSTAHILI ILI KUMUDU
MAISHA YAO.
ANAAHIDI KUBUNI NAFASI MILIONI MBILI ZA KAZI, KWA KUIMARISHA KILIMO
CHA MINAZI, ILI KUSAIDIA NCHI HII KUOKOA SHILINGI BILIONI 50 ZA PESA
ZA KIGENI AMBAZO HUTUMIA KUNUNUA MAFUTA YA NAZI KUTOKA NJE.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,,
0 comments