Open top menu
Wednesday, September 16, 2015
no image

Mchezaji wa Yanga Muyu Twite akishangilia goli lake mara baada ya kuifungia Yanga goli la kwanza kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons

Mchezaji wa Yanga Muyu Twite akishangilia goli lake mara baada ya kuifungia Yanga goli la kwanza kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga imeendeleza wimbi la ushindi katika kuhakikisha inalitetea vyema taji lake baada ya leo kutoa kipigo kingine cha goli 3-0 mbele ya Tanzania Prisons ‘wajelajela’ kutoka jijini Mbeya kwenye mtanange uliomalizika jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa.

Yanga walianza kupata goli la kwanza kipindi cha kwanza kupitia kwa Mbuyu Twite aliyemalizia mpira uliomponyoka mlinda mlango wa Prisons Mohamed Yusuf na kumkuta Twite aliyeachia shuti kali akiwa hatua chache kutoka langoni.
Wakati ikiwa imeongezwa dakika moja ya nyongeza ili mchezo kwenda mapumziko, Amis Tambwe aliifungia Yanga bao la pili baada ya golikipa Mohamed Yusuf kuutema mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na kiungo wa Yanga Thabani Kamusoko na Tambwe kumalizia kwa kichwa na kuifanya Yanga kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa goli 2-0.
Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe akishangilia goli lake
Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe akishangilia goli lake
Kipindi cha pili kilianza kwa Tanzania Prisons kumpumzisha golikipa wao Mohamed Yusuf na kumuingiza Aron Kalambo.
Mshambuliji wa Yanga Donald Ngoma aliihakikishia Yanga ushindi mnono kwa kufunga mkwaju wa penati kufuatia James Josephat kumchezea vibaya Simon Msuva kwenye eneo la hatari. Kutokana na Josephat kumfanyia madhambi Msuva, mwamuzi aliizawadia Yanga mkwaju wa penati pamoja na kumtoa nje Josephat kwa kadi nyekundu.
Wachezaji wa Yanga wakipongezana baada ya kupata bao kwenye mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons
Wachezaji wa Yanga wakipongezana baada ya kupata bao kwenye mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons
Huo unakuwa ni ushindi wa pili mfululizo kwa klabu ya Yanga baada ya kushinda mchezo wake wa awali kwa goli 2-0 dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja huohuo wa Taifa wakati Tanzania Prisons wao wamepoteza michezo yote miwili waliyocheza jijini Dar es Salaam. Walifungwa goli 2-1 na Azam FC kwenye uwanja wa Azam Complex kabla ya leo kuchezea kichapo cha goli 3-0 mbele ya Yanga.
Read more
no image



Mgombea urais wa UKAWA Mh Edward Lowassa ameingia katika mkoa wa Geita kunadi sera za UKAWA na kupata mapokezi ya kishindo yawafuasi wa mabadiliko wakiwemo vijana ambao wamesema harakati zinazofanywa na CCM kumchafua Mh Lowasa hazina nafasi kwani watanzania wamechoshwa na ahadi zisizo na vitendo
 

Mhe. Edward Ngoyai Lowassa akiongea na wananchi wa Chato Geita leo Jumatano 16/9/2015 katika viwanja vya Stendi.

Read more
Friday, February 15, 2013
Hawa ndio wagombea nafasi ya urais nchini Kenya, na sababu ya mwanamama Martha Karua kugombea nafasi hii.

Martha Karua

Martha Wangari Karua

ALIZALIWA TAREHE 22 SEPTEMBA MWAKA 1957 MKOA WA KATI. NA YEYE NDIYE MGOMBEA WA PEKEE MWANAMKE KATIKA UCHAGUZI HUU. ALIAJIRIWA KAMA HAKIMU AKIWA NA UMRI WA MIAKA 24 KABLA YA HATA KUWA MBUNGE MIAKA KUMI BAADAYE.
MGOMBEA WA MUUNGANO WA NATIONAL RAINBOW COALITION (NARC-KENYA), KARUA ALIMTEUA MWANAUCHUMI AUGUSTINE CHEMONGES LOTODO KAMA MGOMBEA MWENZA WAKE. LOTODO PIA AMEWAHI KUWA MBUNGE KATIKA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI
KARUA MWENYE UMRI WA MIAKA 55, ALIKUWA MWANACHAMA WA UPINZANI AMBAO WALIPIGANIA SIASA ZA VYAMA VINGI NCHINI KENYA MAPEMA MIAKA YA TISINI CHINI YA UTAWALA WA RAIS MSTAAFU DANIEL MOI ALIYEKUA ANAONGOZA KIMABAVU CHINI YA CHAMA KIMOJA.
MKEREKETWA WA DEMOKRASIA NA MASWALA YA WANWAKE NCHINI KENYA, KARUA ALIHUSIKA NA KUPIGANIA HAKI ZA WANAWAKE KWA KUTAKA UUNGWAJI MKONO KATIKA MASWALA YANAYOWAHUSISHA WANAWAKE WENYEWE.
Read more
Msanii na Mshiriki wa Big Brother GOLDIE HARVEY  Amefariki Dunia Usiku wa Kuamkia Leo


Habari ya kushtusha iliyotokea usiku huu ni kwamba yule mshiriki wa Big Brother Africa 2012 na mwanamuziki maarufu nchini Nigeria, Goldie Harvey amefariki dunia.

Sio rahisi kuamini kwani Goldie ndo alishaianza safari ya mafanikio ya kuwa msanii mkubwa hapa Afrika na kufanya kazi na baadhi ya wasanii wakubwa ikiwemo Ambwene Yesaya kutoka Tanzania.

Taarifa inasema kuwa Goldie amefariki dunia usiku huu akiwa ndo amerudi kutoka trip yake huko Marekani, chanzo kamili cha kifo cha mwanadada huyu bado hakijawa wazi kwani tukio limetokea kwa ghafla sana usiku wa kuamkia leo.
Read more
Wednesday, February 13, 2013
no image


IMANI ya jamii ya siri ya Freemasons imeonekana kuuteka Mji wa Moshi na vitongoji vyake kutokana na matangazo mengi kubandikwa kila kona yakihamasisha wafuasi kujiunga huku ofa ya utajiri ikipewa kipaumbele.
Risasi Mchanganyiko limeshuhudia matangazo mengi yanayohamasisha kujiunga na imani hiyo yakiwa yamebandikwa kila kona ya mji huu ikiwemo katika nguzo za umeme.
 
Hall la Masonic moshi
Katika tangazo hilo, wahusika wameeleza kwamba watakaojiunga mapema watapewa magari ya kifahari na nyumba za kisasa ikiwa ndiyo njia za awali za kubadilisha maisha yao.
Mwandishi wetu alijifanya anataka kujiunga na kupiga namba za simu zilizowekwa katika tangazo hilo ambazo ni 0783 127 967 ambapo ilipokelewa na mwanaume aliyekataa kutaja jina lake lakini alitoa masharti ya kujiunga.
Read more