Open top menu
Thursday, November 29, 2012

RAIS wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOSO), Paul Yunge, amesema kuwa wanafanya uchunguzi wa kina ili kuwanasa wanafunzi wa chuo hicho wanaojihusisha na biashara ya kujiuza kimwili ili
wawachukulie hatua.

Yunge alifafanua kuwa, wanafunzi watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Yunge alisema kazi ya kufanya uchunguzi tayari imeanza na wanategemea wakati wowote watabaini ukweli kuhusiana na jambo hilo.

Alifafanua kuwa, wanafunzi wanaojihusisha na vitendo hivyo wanakidhalilisha na kukishushia heshima chuo hicho ambacho kimsingi kinapaswa kuwa kioo.

“Ni aibu sana kama watu wamekuja UDOM kusoma na badala yake wanageuka na kufanya biashara ya kujiuza ambayo ni ya kudhalilisha utu wao pamoja na chuo kwa ujumla. Jambo hili lazima tulifanyie kazi,” alisema.

Yunge alidai kuwa wamefikia uamuzi huo baada ya taarifa hiyo kuripotiwa na vyombo vya habari, kitendo ambacho kimeisononesha nchi nzima ukiwemo uongozi wa chuo pamoja na wazazi wa wanafunzi hao.
Tagged
Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments