DAR ES SALAAM, Tanzania
KAMPUNI ya
J-Film 4 Life inayomilikiwa na mwigizaji maarufu wa filamu, Jennifer Kyaka
‘Odama’ inatarajiwa kufanya mapinduzi makubwa ya filamu kutokana na kuwa moja
ya kampuni ambazo zinafanya kazi zake kwa kutumia vifaa vya kisasa.
Akizungumzia
kampuni hiyo iliyoko Kinondoni Biafra, Odama ametoa wito kwa wasanii mbalimbali
wa filamu kwenda kufanya kazi kwa kutumia vifaa hivyo walivyoviingiza mwezi
uliopita.
0 comments