Barnaba akiimba kwa hisia.
Suma Lee akijibu mashambulizi.
MC Jestina akimtambulisha kwenye steji Promota Safina Kassu
Barnaba akifanya makamuzi
Suma Lee akifanya vitu vyake.
Machifu wa Ghana.
Mr & Mrs Chabaka Kilumanga.
Wadau wakiserebuka
---
Salam,
Kassu Ent iliandaa tamasha maalum kutoka kwa
wasanii wetu wa kizazi kipya iliowajumuisha Barbaba na Suma Lee.
Tamasha hili lilikwenda sambamba kwa kusherekea miaka 51 ya Uhuru wa
Tanzania Bara iliyofanyika siku ya jumamosi tarehe 22.12.12 jijini
London katika ukumbi wa Stratford.
Mgeni rasmi alikua naibu Balozi Chabaka Kilumanga
alieambatana na mkewe Irene Kilumanga. Aidha Mh Balozi Kilumanga
aliwapongeza watanzania walioweza kuja kujumuika na kusherekea pamoja
katika siku hii na kuwasihi kuendeleza mshikamano kwa kuishi pamoja kwa
amani na upendo.
0 comments