KIFO cha mwanafunzi Dalton Ott Nyanyika wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
kilichotokea jijini Dar es Salaam hivi karibuni, kimegubikwa na utata kufuatia
ndugu na wazazi wake kudai aliuawa.
Kwa mujibu wa mama mdogo wa mwanafunzi huyo aliyefariki aliyetambuliwa kwa jina la Cesilia Herman, marehemu alikuwa mwaka wa tatu akisomea fani ya Geologia.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu kifo hicho, Cesilia alisema Desemba 5, mwaka huu, walipigiwa simu na wanafunzi wenzake na marehemu na kuwafahamisha kwamba alikuwa anaumwa sana.
Aliongeza kuwa, walipopata taarifa hiyo waliwaomba wakodi gari na kumpeleka nyumbani kwao na walipoona hali yake ilikuwa mbaya wakamkimbiza katika Hospitali ya Mkoa Dodoma.
“Baada ya kuona hali yake inazidi kuwa mbaya, ndugu tulikaa na kuamua kumpeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar kwa ajili ya matibabu zaidi, hata hivyo hakukaa muda mrefu akafariki dunia,” alisema ndugu huyo.

Aidha, mama huyo aliongeza kuwa mazingira ya kifo cha kijana wao yanatia shaka kwa sababu kabla hajafariki walimfanyia uchunguzi na kubaini hakuanguka bali alipigwa na kitu kizito kichwani.
Mama huyo alidai kwamba tukio hilo liliripotiwa katika Kituo Kikuu cha Dodoma... yaani polisi kati na kufungua kesi kuhusu suala hilo .
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa Dodoma, ACP David Misiime alisema tukio hilo halijamfikia na kuahidi kulifuatilia
chanzo:globalpublisher
0 comments