Akiongea na kipindi cha Power Jams leo, Diamond amesema Ogopa Djs waliofanya video hiyo waliiupload kwenye mtandao wa Youtube ili wamtumie link Diamond na uongozi wake waione kama iko sawa ili wakabidhiwe.
Amesema aligundua kuwa kuna kosa katika title ya producer ambayo imeandikwa ‘Wasafi Entertainment’ badala ya Marco Chali na akawataka wabadilishe. Hata hivyo Ogopa walisema wasingeweza kuitoa hiyo ya kwenye Youtube kwa kudai kuwa wangepoteza viewers ila watabadilisha version ya kusambaza kwenye TV.
Hata hivyo Diamond hakukubaliana na wazo hilo na kusisitiza kuwa waiondoe kwanza kwenye mtandao na ndipo Ogopa waliitoa japo walikuwa wameshachelewa kwakuwa kuna watu walikuwa wameidownload tayari na kuiupload kwenye akaunti zao.
Amesema video yenyewe itatoka rasmi Ijumaa hii na bado yeye na uongozi wake wapo kwenye mazungumzo ya iwapo audio yake itoke sasa ama baadaye.
Na hizi ndio screen shots 20 bora za video hiyo.
Party baada ya wazazi kumkubai mchumba wa Diamond
Bata
She is hot au sio?
0 comments