Ijumaa msanii Jaffarai naye alipigwa baadhi ya vifaa vya gari usiku
nyumbani kwao mitaa ya Kijitonyama.Kwenye picha ndo jinsi gari hilo aina
ya Harrier linavyoonekana baada ya kuchomolewa vitu ambavyo Jafarai
anasema kuwa ni Side mirror na Power Window gharama ya vitu vyote ni
laki 8.Jaffarai anasema kuwa mpaka sasa hajapata vifaa hivyo.
Msanii huyo alisema kuwa toka Ijumaa amekuwa akifanya jitihada zakupata
vifaa hivyo kwa kuuliza uliza lakini hajafanikiwa mpaka sasa.Alisema
anachokifanya ni kujipanga kununua vifaa vingine ili aweze kutembelea
gari lake aendelee na mishe mishe zake.Hivi akaribuni pia msanii
mwingine Mh Temba aliibiwa baadhi ya vifaa kwenye gari lake aina ya
Verosa ambavyo navyo alivinunua hivyohivyo kwa kilo 8.
Muenekano wa Gari la Jafarai kabla halijapigwa tukio, likiwa kwenye Car Wash yake 'Jaffarai CarWash' illiyopo pande za Oilcom Mikocheni.Jaffarai wiki iliyopita pia alisema kuwa ameanza biashara ya kusafisha nyumba so kwa yeyote atakyehitaji huduma hiyo amcheki ofisini kwake Jafarrai Car Wash.
0 comments