MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo Ommy Dimpoz anayetamba na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Me & You’, amsema kuwa baada ya video zake mbili ‘Baadaye’ na ‘Nai Nai’, kufanya vizuri sasa anajipanga kuja na utofauti mwingine wa video zake katika ngoma hiyo mpya aliyomshirikisha mwanadada mrembo Vanessa Mdee ambayo amedai mamilioni ya pesa yatatumika.
Mwandishi wetu alizungumza na msanii huyo ili kujua anajipanga vipi na ujio wa video hiyo, ambapo alidai kuwa kila kitu kinakwenda vizuri na kikubwa ni kwamba anataka kuhakikisha kazi hiyo inakuwa na utofauti mkubwa na itatoka mapema January.
“Napenda kuwapa habari fupi mashabiki wangu kwamba video ya ngoma yangu hii mpya itakuwa hewani mapema January hata hivyo nahakikisha inakuwa kwenye kiwango kikubwa ili iweze kufanya vizuri hata kwenye channel kubwa za mziki kama MTV, Channel O na nyinginezo,” alisema.
Hata hivyo Ommy aliongeza kuwa bado hajajua bajeti kamili ya video hiyo kwani sasa ndo wako katika mchakato wa kupanga.
0 comments