Open top menu
Wednesday, January 23, 2013



HALI ya msanii wa maigizo Tanzania anayejulikana kwa jina la Matumaini  si ya kuridhisha kutokana na kusumbuliwa kwa maradhi akiwa nchini Msumbiji

Kutokana na hali yake ya kiafya kuwa mbaya baadhi ya watanzania waishiyo Msumbiji wajitolea kumchangia nauli ili aweze kurejea nyumbani kwa ajili ya kupata matibabu na uangalizi zaidi wa ndugu zake


Akizungumza jijini Dar es Salaam mjumbe wa Bodi Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni , Kaftany Masoud alisema kuwa amepokea taarifa juu ya ugonjwa wa msanii huyo ingawa haijawekwa wazi anasumbuliwa na tatizo gani mpaka sasa


Alisema kutokana na hali kuwa mbaya baadhi ya watanzania wameamua kumchangia msanii huyo ili aweze kurejea nyumbani ili taratibu za matibabu zifwatwe


"Ni kweli hali ya msanii mwenzetu si nzuri anaumwa na unajua ugonjwa wa mtu unathibitishwa na Dokta hivyo bado hatujajua anaumwa nini ila tumeipokea taarifa hiyo na uhudi zinazofanywa ili kumrudisha nyumbani " alisema Masoud



Aliongezea kuwa kwa upande wao kwa sasa wapo katika mchakato wa kuchangishana fedha kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo atakapofika hapa nchini


Matumaini ni msanii kwenye upande wa uchekeshaji alianza kazi hiyo katika kundi la Kaole na kujipatia umaarufu kwa kuigiza na msanii mwenzie Kiwewe

SOURCE:PRO24 
Tagged
Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments