Serikali ya Malawi leo imetangaza kuwa inaiuza ndege ya Rais wa nchi hiyo Joyce Banda katika jitihada zake kukusanya mapato inayoyahitaji.Ndege hiyo yenye miaka 15, nzima NA inauzwa kwa dola milioni 13.3.
Ndege hiyo ni aina ya Dassault Falcon 900EX, imetengenezwa mwaka 1998 na ina seats 14.Rais wa zamani wa Malawi hayati Bingu wa Mutharika aliinunua ndege hiyo miaka mitano iliyopita licha ya nchi hiyo kukabiliwa na umaskini mkubwa.
Kipindi hicho Mutharika alisema ndege hiyo ilikuwa rahisi kuihudumia licha ya nchi hiyo kutegemea misaada ya karibu nusu ya bajeti yake.
0 comments