Open top menu
Tuesday, January 1, 2013





Kwa mujibu wa habari zilizochafua vyakutosha katika mitandao mbalimbali duniani zikimuonesha kuwa ni mtu wa ovyo, mrembo huyo mwenye miaka 29 alizaliwa na mama Mtanzania na baba Mswidishi Septemba 27, 1981.


Ilielezwa kwamba, Ida alianza ‘kamchezo hako ka aibu ka kusimama’ mbele ya kamera za majarida mbalimbali nchini humo yanayolipa vizuri akiwa mtupu tangu mwaka 2008 ambapo aliibuka kinara wa picha ‘mbofumbofu’ wa Machi katika jarida maarufu la Playboy la Marekani.


Habari zikazidi kutiririka kwamba, bila kujali kuwa anachafua jina la Tanzania kimaadili, Ida ambaye hujitambulisha majukwaani kuwa anatoka Tanzania, mwaka 2009 aliibuka tena kinara na safari hiyo hakuwa wa mwezi bali wa mwaka.
Ilielezwa kuwa, Ida ni modo wa kwanza wa Kiafrika kuibuka kinara wa picha hizo kwani inaaminika kuwa siyo rahisi kwa msichana kutoka barani Afrika kuwa na ujasiri wa kukaa utupu.


Habari hizo ziliweka kweupe kwamba, Ida alivumbumbuliwa na kinara wa picha hizo nchini humo mwaka 2007, Sara Jean Underwood huko Beverly Hills, California.


IDA AMEFIKAJE HAPO ALIPO?
Taarifa za Ida zinaonesha kwamba, kutokana na safari za baba yake aliyekuwa akifanya kazi katika Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF), mrembo huyo mwenye uwezo wa kuzungumza Kiswahili, Kiingereza na Kiswidishi alipata ‘chansi’ ya kuzunguka na ‘BABA’ yake duniani na kuona mambo mengi hivyo akajitumbukiza kwenye umodo.





Ilidadavuliwa kwamba, baada ya kuhitimu digrii ya Urembo na Masoko, sasa anajipanga kusomea Uchumi.


Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments