Open top menu
Tuesday, January 1, 2013

KATIKA hali isiyo ya kawaida, kichanga cha siku sita cha jinsi ya kike kimekutwa kimetelekezwa na mtu asiyefahamika juu ya mti ambapo kiliokotwa na mpita njia katika kijiji cha Losimingori kwa Laoshiye, wilayani Arumeru,  ambapo kilikuwa kumeviringishwa kwenye mfuko wa plastiki.
Kitoto kichanga kilichokutwa juu ya mti.
Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Shongon Leswaki Mayo, kichanga hicho kilikutwa hivi karibuni saa 12 jioni na mpita njia aliyetajwa kwa jina la Neema Papalang wakati akipita eneo hilo na kushtuka kuona mtoto analia juu ya mti bila kuwepo mwangalizi yeyote.
Alisema baada ya tukio hilo, msamaria huyo alitoa taarifa kwa uongozi wa eneo hilo mbapo yeye na viongozi wengine walifika na kushuhudia kichanga hicho ambapo kilionekana chenye afya njema.
Aidha, mtendaji huyo alisema kuwa haikufahamika mara moja mtu aliyehusika na  unyama huo wa kikitelekeza kichanga hicho ambapo pamoja na mambo mengine uongozi uliamua kumkabidhi mwanamke huyo kwa lengo la kukihudumia huku taratibu zaidi za kumsaka mama yake zikiendelea.


“Uongozi wa kijiji unaandaa utaratibu wa kukipeleka hospitali ili kuchunguza afya yake. Tukio hilo limewashtua wakazi wa eneo hili ambao ni jamii ya wafugaji,”
alisema mtendaji huyo na kuongeza kuwa wanafanya msako katika eneo hilo na jirani kuweza kumbaini mwanamke yeyote aliyekuwa na ujauzito hivi karibuni na atakayebainika kufanya unyama huo atachukuliwa hatua za kisheria.
Tagged
Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments