Open top menu
Saturday, January 26, 2013

fullKampuni ya Multichoice hivi karibuni ilitangaza kuanza kupokea maombi ya vijana wanaopenda kushiriki shindano la Big Brother Africa ambapo fomu zinapatikana kwenye mtandao. Kuanzia February 1, fomu hizo zitakuwa zikipatikana kwenye ofisi za Multichoice katika nchi zinazoshiriki ikiwemo Tanzania.
Japo shindano hilo hupokea maombi kutoka kwa watu wa aina mbalimbali wakiwemo mastaa na wasio mastaa, hawa ni mastaa 10 ambao tunahisi wanaweza kuwa wawakilishi wazuri. Tumechagua majina haya kwa kuzingatia kigezo kikubwa cha uwezo wa washiriki katika kuongea lugha ya Kiingereza kwa ufasaha.
Wema Sepetu
Wema-sepetu
Mwaka jana mrembo na muigizaji huyo alitweet, ““Dah eti nafaa kuwa next housemate BBA….?”. Tweet hiyo ilipokelewa kwa majibu chanya zaidi kama “Not only kufaa u deserve to be there Wema coz unakismati cha kupendwa na watu,” na kuashiria kuwa Wema anaweza kuwa mwakilishi mzuri. Kwa hakika Wema Sepetu akiamua kushiriki kwenye shindano hilo anaweza kufanya wonders kutokana na haiba yake. Big Brother Africa loves drama and Wema has what it takes to entertain.
Ni msichana ambaye kama akishiriki kwenye shindano hilo, ndani ya muda mfupi anaweza kuwa housemate anayependwa zaidi na Africa.
Wema ni msichana asiyeogopa kuongea yale atakayo kuongea hata kama atatofautiana na wengine. Ukiongezea sauti yake nyembamba kama ya mtoto ambayo ni kivutio kwa wapenzi wa filamu nchini, anafit sana kuiwakilisha Tanzania ambayo kwa mwaka jana ilifanya vibaya kwenye shindano hilo.
Maribeth Vuhahulla aka Lady Ha Ha
220623_4297823560586_386320622_o (600x800)
Maribeth ni mtangazaji wa kipindi cha The Weekend Chatshow cha Clouds TV. Ni msichana mdogo lakini uwezo wake katika utangazaji ni wa kipekee. Anaujua muziki na katika muda mfupi tangu aingie Clouds TV, jina lake limevuma kwa kasi. Hatuna uhakika kama ni mtanzania, lakini kama ni mzawa, anaweza kuwa mwakilishi mzuri.
Shaa
555613_10151437701520051_744930012_n
Sarah Kaisi ana kila sifa za kuwa mshiriki mzuri. Video zake zimewahi kupata nominations kwenye tuzo za Channel O hali inayomfanya ajulikane si Afrika Mashariki tu bali zaidi ya hapo.
Feza Kessy

feza
Mrembo huyo aliyewahi kuwa Miss Dar city centre na sasa akiwa ameingia kwenye muziki, ni mcheshi na kama ukiwa karibu naye huwezi kuboreka. Ana kila sifa za kuingia mjengoni.
Lisa Jensen

Lisa-Jensen
Lisa ni msichana mwingine mrembo ambaye huwezi kumwangalia mara moja ukatosheka. Hatuna uhakika na jinsi anavyojichanganya na watu lakini muonekano na ustaa wake unampa nafasi nzuri ya kuwa mshiriki wa kumfikiria.
Cpwaa
259994_4686339244047_624109040_n
Video zake hususan Problem na Mhmm ambazo ziliwahi kutajwa kwenye tuzo za Channel O, zimempa jina Ilunga Khalifa aka Cpwaa barani Afrika. Ukiongeza na uwezo wake wa kujieleza kimombo, anaweza kuwa mshiriki poa.

Reuben Ndege
ndege
Reuben Ndege aka Nchakalih aliyewahi kuwa mtangazaji wa Clouds FM, ana sifa nyingi za kuwa mshiriki mzuri ndani ya jumba la Big Brother. Kama ukimfollow kwenye mtandao wa Twitter utagundua ni kwa kiasi gani anaulewa mkubwa wa tasnia ya burudani ya ndani na nje ya nchi.
Hemedy
BA_9s2PCMAAlpUW.jpg large
Mwaka jana kulikuwa na uvumi kuwa Hemedy angekuwa mmoja wa wawakilishi wa Tanzania lakini hazikuwa kweli. Bado mwanamuziki na muigizaji huyo wa filamu ana nafasi ya kuwa mshiriki wa BBA kutoka Tanzania. Kama akiziepuka tabia za ubishoo alizozionesha kwenye shindano la Tusker Project Fame jijini Nairobi, BBA inaweza kuwa sehemu nzuri kwake kuongeza umaarufu wake barani Afrika.
TID
tid
Khalid Mohamed aka TID ana vigezo kadhaa vinavyoweza kumfanya awe mwakilishi mzuri. Hatuna uhakika sana na uwezo wake katika kuongea Kiingereza kwa ufasaha lakini mara nyingi interview ameonekana akikichapa poa.
Nisher
nisher
Nisher ni director wa video kutoka Arusha anayekuja kwa kasi nchini. Ni muimbaji, mtunzi na mtayarishaji wa muziki pia ambaye amesomea fani hizo nchini Marekani. Ana muonekano wa kistaa ambao unampa advantage ya kuwa kivutio cha watu.
source:Bongo5
Tagged
Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments