Open top menu
Friday, January 25, 2013




MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya amezua jambo baada ya mume wa mtu, mkazi wa Kata ya Kwadelo wilayani Kondoa, Dodoma ambaye jina lake halikupatikana, kushindwa kuficha hisia zake za kimahaba na kuonesha waziwazi kumzimikia staa huyo.

Tukio hilo lilishuhudiwa na mwanahabari wetu hivi karibuni ambapo Uwoya alikutana na mwanaume huyo kijijini Kwadelo alipokwenda na wasanii wenzake, Jacob Steven ‘JB’ Wema Sepetu, Single Mtambalike ‘Richie’ na Vincent Kigosi ‘Ray’ kuzindua mradi wa Kilimo Kwanza Ajira kwa Vijana kwa mwaliko wa diwani wa kata hiyo, Omary Kariati.

Baada ya kupata nafasi ya kumuona Uwoya uso kwa uso katika maisha yake, mwanaume huyo alifanya jitihada za hali ya juu kujipenyeza katikati ya wanakijiji wenzake na kwenda kuweka pozi na staa huyo kisha kupiga naye picha huku akimkagua kuanzia ukucha hadi unywele.

Kama hiyo haitoshi, baada ya kugundua kuwa Uwoya ni mtu wa kawaida tofauti na alivyomfikiria, alianza kumchezea nywele zake kimahaba huku akitamani kuambatana naye kila alipokuwa akielekea kijijini hapo.



Kwa mujibu wa wanakijiji wenzake, jamaa huyo alikuwa akitamba kuwa alimtaka Uwoya awe mkewe wa pili lakini aliishia kucheka tu bila kumkubalia wala kumkatalia kwa kuwa alimchukulia kama shabiki wake wa kawaida tu.

Katika tukio hilo, mbali na kuzindua Kilimo Kwanza, wasanii hao na Diwani Kariati, pia waliwakabidhi wanakijiji hao Sh. laki tano zilizotolewa kama pole na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Benard Membe kufuatia kijiji hicho kukumbwa na maafa ya mafuriko hivi karibuni

Tagged
Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments