1990-
Nelson Mandela aliachiwa huru kutoka gereza la Victor Verster nje
kidogo ya Cape Town South Africa baada ya kufungwa kwa miaka 27 kama
mfungwa wa kisiasa.
Nelson
Rolihlahla Mandela alizaliwa tarehe 18 Julai mwaka 1918. Ni rais wa
kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini,Alikuwa ni
mwanasheria na mwanachama wa ANC aliyepinga siasa ya ubaguzi Afrika
Kusini, Mandela alitumikia kifungo kutokana na harakati zake za kupinga
ubaguzi wa rangi,
alifungwa katika kisiwa
cha Robben, baada ya kuachiwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya
maridhiano, mwaka 1993 pamoja na Frederik Williem de Klerk alikuwa
mshindi wa tunzo ya amani ya Nobel.
0 comments