KATIKA
kuhakikisha ari ya wachezaji inarudi kama ilivyokuwa mwanzo, uongozi wa
klabu ya Simba una mpango wa kuipeleka timu nje ya nchi ili kuwapa muda
wachezaji wa kusahau yaliyopita na kujipanga vema kwa mzunguko wa
pili.
Aidha,
uongozi wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Vodacom, umemuomba radhi
kipa na nahodha wake, Juma Kaseja kutokana na kudhalilishwa na baadhi
ya watu baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo usioridhisha katika michezo
yake ya mwishoni mwa mzunguko wa kwanza.
Mwenyekiti
wa Simba, Ismail Aden Rage amesema leo kwamba kudhalilishwa kwa Kaseja
si sahihi kwani anaweza kukofanya makosa ya kiufundi kama binadamu
mwingine, hivyo anahitaji ushauri wa kimawazo.
“Tuache
kudhalilisha wachezaji kwani kufanya hivyo si uungwana wa michezo hata
kidogo…kila mtu anafahamu kuna kushinda, kufungwa na kutoka sare, kama
hatutaki kufungwa tujiondoe wenye ligi,”alisema Rage
0 comments