Afsa Kazinje Atua Bongo kutoka Majuu na Zawadi Hii
Malkia wa muziki wa kizazi kipya pamoja na zouk Hafsa Kazinja anarudi leo nchini Tanzania baada ya kumaliza ziara yake ya miezi mitatu nchini marekani na leo atawasili Dar-Es-Salaam na ndege ya Shirika la South African Airline.
Kwa mujibu wa Promota wa msanii huyo, bwana Dickson Mkama kutoka Marekani ametuma taarifa hii kwa watanzania ili wampokee kwa shangwe pamoja na kumuunga mkongo kwa kile alicho tuletea,
Hafsa aliweza kurekodi nyimbo mpya na mpiga gitaa maarufu kutoka zaire “NgumaLlokito…na aliweza kufanya video ya wimbo huo na madansa wa kizungu ambao waliupenda sana wimbo huo unaoitwa “songa mbele”
Aidha promota huyo aliwaomba wapenzi, wadau na mashabiki wa msanii huyo kujitokeza kwa wingi na kumpokea msanii huyo ambaye ana zawadi ya video yake mpya ambayo inakwenda kwa jina Songa mbele.
Related Posts
- Ney wa Mitego: ‘Siwezi kumjibu Nikki Mbishi, naweza nikamlea yeye na akaishi vizuri na kumkodishia salon ya kusuka’
- Kampuni ya Steps Entertainment ya jijini Dar es Salaam imeingia kwenye Kashfa Nzito ya Kutumia Hirizi Mlangoni kwa ajiri ya Kuwazima wasanii
- Picha Mbalimbali zikimuonesha Chris Brown akisindikizwa Mahakamani na Rihanna kwenye Kesi inayoendelea Mahakani
0 comments