MSANII
wa filamu na muziki Snura Mushi ‘Snura’, anayetamba kwa mauno, ameeleza
kuwa mwaka huu anaamini ni mwaka wake wa kukimbiza kutokana na mapokezi
makubwa anayoendelea kuyapata kutoka kwa mashabiki wake hasa kwenye
show zake.
Snura
alizungumza na mwandishi wa DarTalk, ambapo alisema kuwa muziki wake
umeedelea kumweka juu, na anaamini ujio wake wa mwaka huu kila msanii
anayemfuata nyuma yake atasubiri kwani anajua kile anachokifanya kwa
akili ya mashabiki wake.
Hata
hivyo alisema kuwa anatarajia kuzindua rasmi video yake mpya ya
‘Majanga’ kwenye usiku wa Viuno Show ndani ya New Maisha Club Jumapili
hii ambapo pia atasindikizwa na wakali wengine kibao.
“Nafanya
muziki na filamu na huwezi amini mashabiki wangu wamekuwa wakipokea kwa
shangwe sana pale napoenda kufanya show, naamini huu mwaka kwangu
utakuwa na mafanikio makubwa sana tofauti na nyuma,” alisema. Toa Maoni
yako Hapa chini
0 comments