MAMA wa staa wa songi la Kesho, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim, amewakataa mademu wote waliodaiwa kutembea na mwanaye kwa kusema hakuna kati yao anayemtambua kama mkwe wake.
Akipiga stori na paparazi wetu juzikati jijini Dar, Bi’ mkubwa huyo alisema amechoshwa kusikia mademu kama Wema Sepetu, Jokate Mwegelo na Penny wakinadiwa kuwa ni wachumba wa mwanaye wakati yeye huwa wanamuomba kupiga naye picha kama mashabiki wengine.