Chris Brown amewaomba radhi fans wake kwa picha yake
aliyopost kwenye instagram hivi karibuni ikimuonesha akijipeleka higher na
marijuana.
‘Don’t wake me up
hit maker’ alikuwa criticised sana na watu baada ya ku-upload picha
akivuta misokoto mitatu ya marijuana a.k.a weed kwa wakati mmoja
alipotembelea kijiwe kimoja cha wavuta bangi na baadae kupiga picha
ambazo aliziweka akiwa na marafiki zake wa kijiweni hapo.
Breezy ambae alipost picha akiwa katika ziara yake huko Nertherlands,
alifunguka kupitia twitter baada ya watu kuponda sana picha hiyo, tweet yake
inasomeka “Oh Amsterdam, wote mnani-treat vizuri sana, namuomba radhi kila
mmoja ambae alijisikia vibaya kwa picha yangu ya bangi.” Aliandika Breezy .
Akaona kama haitoshi ikabidi atoe na ushauri pia, “naomba
radhi kila mtu lakini kama wote hampendi basi msifanye hivyo pia. Ni rahisi.”
Breezy ambae hivi karibuni ameirudia account yake ya twitter
baada ya kuitelekeza kwa muda mrefu kwa sababu ya mgogoro wake na mchekeshaji
Jenny Johson, hivi karibuni alitweet message ya kwanza akimaanisha he is back
again kwenye mtandao huo wa kijamii na anaanza upya, “ Time to start fresh.
#newchapter.” Ilitweet Chris Brown.
Mkali huyo wa R&B aliwashauri pia watu wake ‘team Chris
Brown’ kutumia vizuri account ya tweeter kwa kusapoti na kuuza muziki wake na
sio kuzungumzia mambo ya relationship abuse.
0 comments