Mario Balotelli
'mtoto mtukutu' sasa anarudi kwao rasmi baada ya Manchester City
kukubaliana bei na AC Milan juu ya kumnunua mchezaji huyo jioni hii.
Juventus nao
walionyesha nia ya kumtaka Balotelli lakini wamekubali ofa ya £17
million kutoka kwa AC Milan huku kukiwa na nyongeza ya £2.5m
itakayotolewa kulingana na mafanikio ya mchezaji. Balotelli anatarajiwa
kwenda Italy kwa ajili ya vipimo vya afya kesho na kusaini mkataba wa
miaka minne na nusu.
Balotelli pia
amesadia dili hilo kukamilika baada ya kukubali kukatwa kiasi cha £1m
ili aweze kujiunga na klabu yake ya utotoni kwa mkataba wenye thamani ya
£3m.
0 comments