Young
Africans leo imeendeleza wimbi lake la ushindi katika mzunguko wa pili
wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa tmu ya Tanzania Prisosns kutoka
mjini Mbeya jumla ya mabao 3-1, katika mchezo uliofanyika jioni hii
katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young
Africans ambayo inaongoza ligi kwa kuwa na pointi 32 na mabao 28 ya
kufunga, iliingia uwanjani kwa ajili ya kusaka pointi 3 muhimu ambazo
imefanikiwa kuzipata.
Kikosi
cha mholanzi Ernest Brandts kiliuanza mchezo kwa kasi, na kupata bao la
kwanza dakika ya 11 kupitia kwa Jerson Tegete aliyemalizia pasi safi ya
kiungo mshambuliaji Saimon Msuva.
Dakika
sita baadae dakika ya 17, mshambuliaji wa Elias Maguli aliipatia
Prisons bao la kusawazisha kufuatia uzembe wa walinzi wa Yanga kuzembea
kumkaba mfungaji aliyekokota mpira toka upande wa pembeni mpaka
alipofunga bao hilo.
Didier
Kavumbagu alikosa mabao ya wazi dakika ya 7 na dakika 27 huku kiungo
Nurdin Bakari akikosa pia bao la wazi dakika ya 38 ya mchezo.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza Young Africans 1-1 Prisons FC.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi na Yanga kuutawala mchezo hali iliyopelekea
kujipatia bao la pili kupitia kwa mlinzi wa kulia Mbuyu Twite
aliyemalizia mpira uliokolewa na walinzi wa Prisons kufuatia piga
nikupige ya Nadir Haroub, na Saimon Msuvalangoni mwa lango la Prisons
kabla ya mpira huo kumkuta Twite aliyeukwamisha wavuni.
Jerson
Tegete aliendelea kuwa mwiba kwa timu ya Prisons baada ya kuipatia
Young Africans bao la tatu dakika ya 66, akimalizia pasi safi ya kiungo
Nurdin Bakari aliyetanguliziwa mpira na Hamis Kiiza na Nurdin kuwatoka
walinzi wa Prisons kabla ya kumpasia Tegete aliyeukwamisha mpira wavuni
bila ya ajizi.
Kama
washambuliaji wa Young Africans wangekuwa makini Yanga ingeweza kuibuka
na ushindi wa mabao mengi kwani Jerson Tegete alikosa bao la wazi baada
ya kuwapinga chenga walinzi wote wa Prisons lakini umaliziaji wake
haukuwa mzuri.
Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 3- 1 Prisons FC
Kiungo
Frank Domayo aliugua ghafla na kuondolewa katika orodha ya wachezaji ya
waliokuwa katika listi ya kuanza na nafasi yake ilichukuliwa na Nurdin
Bakari, Domayo alijisikia kizunguzungu hali iliyompelekea daktari wa
timu ya Yanga Dr Nassoro Matuzya kufukiria huenda akawa na malaria,
baadaye Domayo alijisikia nafuu na kuutazama mchezo wote kwa dakika 90.
Kocha
mkuu wa Yanga Ernest Brndts amesema anashukuru timu yake kupata kwa
ushindi katika mchezo wa leo, kipindi cha kwanza wachezaji wangu
hawakuwa makini na hawakuzingatia maaelekezo yangu , lakini wakati wa
mapumziko niliwaeleza nini wanapaswa kukifanya na hatimaye timu
ilibadilika na kuweza kutengeneza nafasi za kufunga mabao mawili
japokuwa walikosa nafasi zingine za wazi
Kambi
yetu ya mafunzo nchini Uturuki imetusaidia sana, wachezaji wanacheza
kwa kujiamin ila kuna mapungufu madogo madogo yalijitokeza katika mchezo
wa leo, benchi la ufundi tumeyaona na tutayafanyia kazi katika michezo
itakayofuata alisema "Brandts"
Young
Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Mbuyu Twite/Juma Abdul, 3.Oscar
Joshua, 4.Nadir Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd
'Chuji', 7.Saimon Msuva, 8.Nurdin Bakari/David Luhende, 9.Didier
Kavumbagu/Hamis Kiiza, 10.Jerson Tegete, 11.Haruna Niyonzima
Dkt. Steven Ulimboka, akijumuika na mashabiki wenzake wa Yanga jukwaani, wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao la Mbuyu Twite.
Kikosi cha Prisons kilichoanza leo |
Kikosi cha Yanga kilichoanza leo |
Didier
Kavumbangu akimtoka beki wa Prisons Jumanne Elfadhil katika mchezo wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam jioni hii. Yanga ilishinda 3-1.
|
Kavu amepiga krosi baada ya kupata mwanya |
0 comments