Kwa
muda mrefu matajiri wengi walitamani kulinunua jumba la kifahari la
marehemu Michael Jackson ambalo pia linakumbukumbu kubwa kwa kuwa ndipo
alipofia mfalme huyo wa Pop, sasa jumba hilo limepata mnunuzi na
limeshalipiwa mkwanja wote unaostahili.
Kwa
mujibu wa mtandao wa TMZ jumba hilo limenunuliwa na Steven Mayer ambae
ni tajiri mkubwa na muwekezaji katika masuala ya bank.
Vyanzo
mbalimbali vinaonesha kuwa jumba hilo limeuzwa kati ya dola za
kimarekani million 17 na dola million 20, na lilikuwa limepangwa kuuzwa
karibia dola za marekani million 24, ambazo zikibadilishwa kwa shilingi
za kitanzania yatakuwa mabilioni kibao.
Inaonesha
kuwa mnunuzi huyo anahamu kubwa ya kuingia katika jumba hilo kiasi
kwamba amehamia wiki moja kabla ya umiliki wa mtu aliyekabidhiwa
kuiangalia haujafungwa rasmi.
Kinachofurahisha
zaidi ni kwamba muuzaji nae amemruhusu Mayer ahamie kwenye jumba hilo
hata kabla hajasitishiwa rasmi umiliki ama uangalizi wa jumba hilo la
kifahari, japokuwa anasitasita kwa kuwa anaona ni risk kwake.
Steven
Mayer anaonekana analipenda sana jumba hilo kati ya matajiri wengi
ambao walikuwa wanalitamani jumba hilo kwa hiyo kwa bei yoyote alikuwa
tayari kulinunua na kushare baraka za Michael Jackson kwenye mjengo huo.
Imeandikwa na Leo Tainment
0 comments