Open top menu
Sunday, November 4, 2012


Nyota wa filamu ambaye pia ni mtangazaji wa kituo kimoja cha runinga nchini Christine Manongi ‘Sintah’, amekanusha vikali uwepo wa picha zake za utupu na kudai kuwa anayesema anazo basi aziweke hadharani ili watu waone ujinga wake ingawa anaamini kuwa katika maisha yake hajawahi kupiga picha za namna hiyo kama watoto wadogo wanavyofanya. Lipo kundi la watu kadhaa linalodai kuwa wana picha za msanii huyo zinazomuonesha mwili wake ukiwa mtupu kama alivyozaliwa huku ikidaiwa kuwa picha hizo alipigia nchini Marekani na baadhi yake zilitumika kwenye movie kadhaa za utupu.
Tetesi za kuwepo kwa picha za utupu za Sintah zimezidi kuzagaa mitaa hivi sasa huku watu kadhaa wanaodai kuwa nazo wakiapa kumlipua  msanii huyo kama ataleta  zake  ambapo  katika mazungumzo aliyofanya na teentz.com sintah alidai kuwa anasikia watu wakisema kuwa wana picha zake za utupu lakini kwa upande wake anaamini katika maisha yake hajawahi kupiga picha za namna hiyo pengine apigwe na mpenzi wake bila yeye kujua.

Alisema kuwa mara nyingi safari zake za nje huwa si kwa ajili ya kufanya upuuzi kama huo bali anaenda kwa ajili ya kazi hivyo baadhi ya watu wanaona wivu na ndiyo maana wanazusha habari ambazo hazileti picha nzuri kwani jamii.

“Mimi ni jeshi la mtu mmoja hivyo wanapoona mafanikio yangu yanakuja wanaanza kuleta habari zao za kumchafua mtu, nawaambia tu kwamba sitishiki na nitazidi kusonga mbele na hao wanaosema hivyo watabaki na umaskini wao,” alisema.
Tagged
Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments