Mbunge
wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe akichangia kwa hisia katika semina ya
wabunge juu ya fao la kujitoa, kwenye ofisi za bunge mjini Dodoma leo.
Wabunge
wa bunge la Tanzania wamegawanyika katika semina yao juu ya fao la
kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii ambapo wabunge wengi vijana
wanataka mifuko hiyo irudishe sheria ya kujitoa wakati mawaziri na
baadhi ya wabunge wengine wanakataa kurudishwa kwa fao hilo.
Kuna
hoja zingine za wabunge zinazotaka sheria ya fao la kujitoa lisiwepo
na badala yake kuwepo fao lingine la kujikimu kwa wanachama
wanaoachishwa kazi wakati wakisubiri umri wao wa kupata fao la kujitioa.
Mbunge
wa Kigoma Kaskazini Zito Kabwe (Chadema) amesema kuwa kwa sasa fedha
nyingi za mifuko ya hifadhi ya jamii zinatumika vibaya kwa kisingizio
cha uwekezaji na masuala mengine yanayofanana na hayo na kusababisha
hofu kubwa ya uwezo wa mifuko hiyo kuwalipa wanachama wake hapo
baadaye.
Amesema
kuwa yeye hatakuwa tayari kuona kuwa mifuko hiyo haina fedha ya
kuwalipa wanachama wanaofikisha umri wa kupata fao la kujitoa, endapo
kama atakuwa Rais wa nchi yetu ya Tanzania .
Zito
amesema kuwa hata kama siye yeye atakuwa Rais wa Tanzania miaka ijayo,
laikini hatapenda kuona mtu yeyote atakayekuwa Rais akishindwa kuwalipa
mafao wanachama wa mifuko hiyo.
Usemi
wa Zitto ulileta minong’ono kutoka kwa wabunge na Spika aliyekuwa
anahudhuria semina hiyo katika ukumbi wa zamani wa Bunge kwa sasa
unaitwa ukumbi wa Pius Msekwa.
0 comments