Open top menu
Friday, November 2, 2012


 
Usiku wa kuamkia tarehe 23 mwezi uliopita watu wasiojulikana walilichoma kwa moto gari la Jackline Wolper lililokuwa limepakiwa nyumbani kwake. Hata hivyo gari hili halikuungua lote.


Gari la Jackline baada ya kuchomwa

Kupitia blog yake, Jack ameandika:

Kiukweli mimi kama Jacquline Wolper sina ubaya na mtu yeyote, ila nmeshangaa kuona watu nisiyo wajua kuja usiku wa manane na kunichomea gari yangu. Kiukweli siwezi kumuhisi mtu ila najua ni lazima atakua mtu asiependa maendeleo yangu ni ni mtu mbaya sana kwangu. Na inawezekana kabisa alipanga kunia lakni kwa bahati nzuri siku hiyo sikua nyumbani nilikua nimesafiri. Tukio lilitokea usiku wa tarehe 23/10/2012
ambapo mtu alitumia matambara yaliyo na mafuta ya taa au Petrol akiwa kwa nje ya ukuta wa nyumba yangu akiwa anarusha kwa ndani. Nimepeleka taarifa kituo cha Polisi kawe kwa kutaka msaada wa kiupelezi na nitakua nawapa taarifa za kila kinachoendelea. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwani niko salama.
Tagged
Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments