Open top menu
Friday, January 18, 2013

SIKU chache baada ya kuwepo kwa madai kuwa modo ambaye pia ni Miss Tanzania namba 2, 2006, Jokate Mwegelo amechumbiwa, mwanamuziki mkongwe John Kitime (picha ndogo) ameingiza utani kwenye jambo hilo kwa kumlaumu kulifanya kuwa la siri kama kweli lipo.

Kupitia blog yake mzee Kitime aliandika hivi: “Mimi na Watanzania wenzangu tumepata mshtuko baada ya kusoma habari hii. Mpaka sasa tunajiuliza ‘why Jokate Why?’ 

 
“Wewe unaelewa taratibu kuwa mtu anapotaka kuchumbiwa huwa haifanywi siri.


“Jambo la kwanza unaenda kwa afisa utamaduni kuomba kibali ambacho unatakiwa kukipitisha vituo vya polisi vya jirani kisha kibali hicho kupigwa mhuri na katibu mtendaji wa kata unayotegemewa kuchumbiwa na hatimaye kupitia kwangu Afisa Vibali vya Kuchumbiwa, ambapo nitaita Press Conference kutangaza uchumba. Umevunja sheria namba 6 ya 1956 ya Uchumbalization Act...”
Source:Mpekuzi 
Tagged
Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments