RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Leodegar Tenga amesema kwamba hawezi kugombea tena nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo unaotarajia kufanyika February 24 mwaka huu.
Akizungumza na Waandishi wa habari hivi punde jijini Dar es Salaam, Tenga amesema kwamba wakati anaingia madarakani miaka minne iliyopita alikuwa na kazi ya kufanya, ambayo ilikuwa ni kujenga taasisi ya Soka nchini, na kwamba hawezi kuendelea tena kwani uongozi ni kijiti na kwamba huu sasa wakati wa kukimbizwa na mtu mwingine.
"Nimekaa madarakani kwa miaka minane kwakweli ni miaka mingi sana,tangu mwaka 2004 ambapo wakati huu kulikuwa na ajenda maalum ya kuleta mabadiliko ya msingi katika soka"alisema Tenga.
0 comments