Open top menu
Monday, January 14, 2013

Hali ya hatari ya zidi kupamba moto kwa wanafunzi wanao ishi maeneo ya Kivukoni (Kigamboni ward) in Temeke District, Dar es Salaam. Sasa hivi eneo hilo hasa nyumba na hostel wanazoishi wanafunzi kutoka Chuo cha usimamizi wa Fedha, IFM  na wale wa Mwalimu Nyerere Memorial Academy limekuwa halitamaniki na kutishia amani na kuwekea kikwazo shughuli za wanafunzi hao hasa katika elimu, Matukio ya uvamizi na wizi wa laptop,simu za mikononi na pesa yamezidi kwa kasi sana, Suala lingine ambalo limekuwa la kusikitisha ni lile la ubakaji wa dada zetu, maana imekuwa hatari kwa wanawakewanaibiwa na kubakwa pia,
Style wanayoitumia watu hao ni kuvamia rooms na hostel wakiwa na mapanga huku wamevaa mask usoni, siku si nyingi walivamia hostel iliyopo mtaa wa Mwinyi Hamis,kigamboni na kupora simu na laptop hasa ndio lengo lao kubwa,
Wanacholia wanafunzi ni kutokupata support kutoka serikalini hasa jeshi la polisi lina husika na ulinzi na usalama wa raia na mali zake, kabla sijaingia mtamboni sasa hivi nimepata taarifa kuwa wanafunzi wa IFM wanapanga maandamano ya amani kuelekea kwa mkuu wa polisi Dar es saalam Kamanda Kova,
FOL CLASSIC kupitia UNIVERSITY LENS tuna laani vikali suala hili maana malalako haya haya jaanza kwa wanafunzi hawa, tatizo hili ni sugu vyuoni maana hata wanafunzi wa UDSM wanaoishi Changanyikeni hukubwa na tatizo hili mara kwa mara.

Nini kifanyike juu ya hili
toa maoni yako,kero yako na matatizo au matukio yote ya vyuoni kupitia email yetu 
folclassic@gmail.com
Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments