MSANII kutoka kiwanda cha filamu Bongo, Aunt Ezekiel amefunguka kuwa ana mpango wa kutimka Bongo siku chache zijazo na kumfuata mumewe, Sunday Demonte anayeishi Dubai.
Akiongea na mwandishi wetu, Aunt alisema baada ya kufunga ndoa alikaa Dubai kwa muda mchache na kurudi Bongo kwa ajili ya kuweka mambo yake sawa na akimaliza atarudi kwa mumewe na atakuwa anakuja kwa ajili ya kucheza muvi tu.
“Mimi sasa nimeshakuwa mke wa mtu hivyo ni lazima niwe karibu na mume wangu na ndiyo maana nimekuja kuweka mambo yangu sawa nikimaliza namfuata, Bongo nitakuja kwa msimu tu,” alisema Aunt.
0 comments