AZAM
FC wamefanikiwa kutetea Kombe la Mapinduzi usiku huu kwenye Uwanja wa
Amaan, Zanzibar baada ya kuifunga Tusker FC ya Kenya mabao 2-1.
Kwa ushindi huo, Azam wamezawadiwa Sh. Milioni 10, wakati washindi wa pili Tusker wamepata Sh. Milioni 5.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Ramadhan Rajab Ibada ‘Kibo’
aliyesaidiwa na Mwanahija Makame Mfumo na Mgaza Kindundi, hadi mapumziko
hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao.
Azam
ndio walioshambulia zaidi katika kipindi hicho, lakini hawakuwa na
bahati ya kufunga bao japo moja. Gaudence Mwaikimba alipewa pasi nzuri
na Brian Umony dakika ya 44, lakini shuti lake kali lilidakwa na kipa
Samuel Odhiambo.
Kipindi cha pili, Tusker walirudi na moto mkali na kuanza kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Azam.
Hiyo
iliwasaidia mabingwa hao wa Kenya kupata bao dakika ya 60, lililofungwa
na Jesse Were aliyeunganisha kwa shuti kali la kimo cha mbuzi pasi ya
Robert Omunok.
Hata
hivyo, bao hilo halikudumu sana, kwani Azam FC walisawazisha dakika ya
72 lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na beki Mkenya, Joackins Atudo
baada ya beki wa Tusker, Luke Ochieng kuunawa mpira kwenye eneo la
hatari.
Katika
dakika mbili za nyongeza baada ya kutimu kwa dakika 90 za mchezo huo,
alijitokeza binti mwenye umri kati ya 14 na 16 na kukatiza uwanjani
akitokea jukwaa la Urusi
Refa
alijaribu kumsimamisha, lakini aliendelea kukatiza Uwanja hadi nje
ambako alipokewa na askari Polisi na kutolewa nje kabisa ya Uwanja.
Mtangazaji wa Uwanja wa Amaan, Farouk Karim aliwatuliza mashabiki
akisema binti huyo ametoroka hospitali ya vichaa, Kidongo Chekundu na
tayari Polisi wamemkamata na kumrejesha huko.
Hadi dakika 90 zinamalizika timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1 na ndipo zikaongezwa dakika 30.
Gaudence Exavery Mwaikimba aliipatia
Azam bao la ushindi dakika ya pili tu tangu kuanza kwa muda wa nyongeza
baada ya kuwazidi nguvu na maarifa mabeki wa Tusker.
Kikosi cha Azam leo kilikuwa; Mwadini
Ally, Himid Mao, Samir Hajji Nuhu, David Mwantika, Joackins Atudo, Kipre
Balou, Humphrey Mieno, Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba, Brian
Umony/Malika Ndeule dk126 na Uhuru Suleiman/Seif Abdallah dk64.
Tusker FC; Samuel Odhiambo, Luke
Ochieng, Bright Jeremiah, Martin Kizza, Joseph Shikokoti, Frederick
Onyango/Mark Ochiambo dk93, Andrew Tolowa/Edwin Ombasa dk 55, Khalid
Aucho/Benson Amianda dk 80, Jesse Were/Andrew Sekayambya dk54, Ismail
Dunga/Michael Olunga dk52 na Robert
0 comments