Open top menu
Sunday, January 13, 2013

Career Network Connection(CNC) ni muunganiko wa wanafunzi kutoka UDSM,ARU na IFM lengo ni kuunganisha taaluma mbalimbali ili kuisaidia jamii kutatua matatizo na changamoto zinazoikabili jamii. Jana tarehe 12/01/2013 wanafunzi hao walitembelea pamoja na kushiriki kazi katika kituo cha watoto yatima na wale waishio mazingira magumu, kituo cha SOS kilichopo ubungo(karibu na Mawasiliano tower) ila makao makuu yake ni nchini Australia. Ndani ya Shuttle ni Team nzima ya Career Network Connection (CNC) kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam kuelekea kituoni hapo (SOS)
Baada ya kuwasili kituoni hapo team nzima ya Career Network Connection(CNC) ilikaribishwa katika ukumbi wa mikutano kituoni hapo.
Huyu ndiye Afisa Utawala wa kituo hichi hapa ubungo akitoa shukrani na pongenzi kwa wanafunzi hawa wa Elimu ya juu kwa kile walichokifanya, nakutaka iwe mfano kwa wanachuo wengine kutambua uwepo wa watu kama hao kwani wao ndio viongozi wetu wa leo kesho hivyo ni vema kujihusisha na jamii mapema ili kuzijua changamoto zinazo ikabili jamii.

Hiki ndicho kile kidogo wasomi hawa walichoona ni vema kugawana na hawa watoto, ili kuwapa faraja japo ya sekunde katika maisha yao.
Afisa utawala akipokea msaada toka kwa team ya CNC
Tofauti kubwa iliyoletwa na Career Network Connection  ( CNC ) katika kituo hichi ni utayari wao wakushiriki kila kilichotakiwa kufanywa kwa siku kituoni hapo, kwani walishiriki katika kupika, kula pamoja na watoto hao ni kitu ambacho kilipelekea faraja kubwa kwa watoto hao na walezi wao.

Bila shaka watoto walienjoy
Usafi pia ulihusika kituoni hapo.
baada ya kula na shughuli za usafi sasakilichofuta ni michezo mbalimbali iliyofanywa na watoto hao, it was so funny!

Different Themes
Written by folclassic

Aenean quis feugiat elit. Quisque ultricies sollicitudin ante ut venenatis. Nulla dapibus placerat faucibus. Aenean quis leo non neque ultrices scelerisque. Nullam nec vulputate velit. Etiam fermentum turpis at magna tristique interdum.

0 comments